Connect with us

Habari

Mrithi Wa Mayanja Kutua Dar Leo – Ni Yule Aliyeipa Ubingwa Rayon Sports Msimu Uliopita

Spread the love

INAONEKANA kama Simba wameshapata mrithi wa Jackson Mayanja ambaye hapo jana alibwaga manyanga kama kocha msaidizi wa Simba SC.

Tovuti ya Mwanaspoti inaripoti kuwa Djuma Masudi kutoka Burundi ndio anakuja kurithi mikoba ya Mayanja ambaye ameitumikia Simba kwa miezi 22.

Masudi mzaliwa wa Bujumbura nchini Burundi aliichezea klabu ya Inter FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Burundi sambamba na timu ya taifa akiwa kama mshambuliaji.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 40 amefanikiwa kuipa klabu ya Rayon Sports ubingwa wa Ligi Kuu ya Rwanda msimu uliopita kabla ya kujiuzulu huku akitajwa kuwa mmoja wa makocha vijana machachari na mizuka ya kufa mtu pindi timu yake inapoibuka na ushindi.

Vyanzo vya Mwanaspoti vinadai kuwa uongozi wa klabu ya Simba umevutiwa na mafanikio ya kocha huyo na anatarajiwa kutua leo ili pande hizo mbili ziweze kumalizana kabla ya kuanza majukumu yake kwenye kikosi cha Simba ambacho kinajiandaa na mchezo wa Ligi mwishonu mwa wiki dhidi ya Njombe Mji kwenye dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam.


Spread the love

More in Habari