Connect with us

Habari

Mourinho Kujifunga Miaka Mingine Mitano Manchester United

MANCHESTER UNITED wana mpango wa kumuongezea Jose Mourinhomkataba mpya wa miaka mitano wenye thamani ya paundi milioni 65

Inaelezwa kuwa kocha huyo raia wa Ureno yupo tayari kusaini dili hilo ambalo litamfanya kukaa Old Trafford kwa muda mrefu zaidi kwenye historia yake ya ukocha.

Mourinho ndiye kocha anayeongoza kwa kulipwa vizuri duniani sambamba na Pep Guardiola wa Manchester City ambao wote wanapokea paundi 250,000 kwa wiki.

Kwenye mkataba huo mpya, mshahara unatarajiwa kubaki ule ule wa awali ingawa kutakuwa na nyongeza itakayotokana na makombe anayochukua au nafasi atakayomaliza kwenye ligi.

Mazungumzo yanaendelea kati ya pande hizo mbili ambapo mabosi wa United wanaamini kuwa Mourinho ni kocha sahihi kwao.

Mourinho ambaye ana mkataba wa miaka mitatu  na United aliosaini mwaka jana, aliwawezesha mashetani hao wekundu kutwaa makombe mawili msimu uliopita ya Europa League na Kombe la Ligi huku United kwa sasa ikishikilia usukani wa EPL sambamba na hasimu wake, Manchester City.

More in Habari