Connect with us

Habari

Mayanja Aliomba Kujiuzulu Siku Nyingi Sana -Haji Manara

Spread the love

KLABU ya Simba imetoa ufafanuzi juu ya ujio wa kocha msaidizi mpya wa kikosi hicho ikiwa ni siku moja tu baada ya aliyekuwa amekalia nafasi hiyo, Jackson Mayanja kujiuzulu.

Mayanja hapo jana alijiuzulu kuifundisha Simba kwa sababu zilizoelezwa kuwa ni matatizo ya kifamilia huku mrithi wake, Djuma Masudi kutoka Burundi akitambulishwa rasmi muda mfupi uliopita hali iliyofanya mashabiki kuhoji kitendo cha kupatikana kwa kocha huyo mapema.

Mashabiki hao ambao walionekana kutoridhishwa na sababu ya Mayanja kujiuzulu huku wakiendelea kushangazwa na kitendo cha Simba kumpata mrithi wake ndani ya masaa 24 tangu kutangazwa kujiuzulu kwake.

Muda mrefu

Akitoa ufafanuzi kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye makao makuu ya klabu hiyo jijini Dar es Salaam, Manara alisema:

“Matatizo ya kocha Mayanja yalikuwa ya muda mrefu na alituomba kujiuzulu mapema lakini nasi tulimuomba atuvumilie mpaka tutakapopata kocha mwingine na kumalizana naye.

“Jambo hili tulikaa nalo kwa muda mrefu na ndio maana safari za kwenda Kampala za kocha Mayanja zilikuwa ni za mara kwa mara,” alifafanua Manara.

Masudi aliyetua jijini Dar es Salaam na kutambulishwa rasmi mbele ya waandishi wa habari, ataungana na kocha Mkuu, Joseph Omog na kuanza kazi mara moja ili kujiandaa na mchezo wa Ligi siku ya Jumamosi dhidi ya Njombe Mji utakaopigwa kwenye dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam.


Spread the love

More in Habari