Connect with us

Habari

Matokeo Ya Mechi Zote Za EPL Zilizopigwa Leo Haya Hapa;

Everton's English striker Wayne Rooney (R) celebrates scoring the opening goal during the English Premier League football match between Everton and Stoke City at Goodison Park in Liverpool, north-west England on August 12, 2017. PHOTO/AFP
Spread the love

Ligi Kuu ya Uingereza maarufu kama EPL imeendelea tena leo ambapo vilabu kadhaa vimeshuka dimbaani kutupa karata zao za kwanza.

Kwenye mechi ya mapema iliyopigwa kwenye dimba la Vicarage Road, Watford walitoka sare ya mabao 3-3 na Liverpool ambapo mabao ya Liverpool yamefungwa na Alberto Firminho, Mohamed Salah na Sadio Mane huku yake ya Watford yakiwekwa kimiani na Stefano Okaka, AbdoulayeDoucoure na Miguel Britos

Chelsea wamepokea kichapo mbele ya Burnley kwenye dimba la Stamford Bridge, ambapo mabao ya Burnley yamefungwa na Sam Vokes, Stephen Ward na Sam Vokes huku yale ya Chelsea yakifungwa na Alvaro Morata pamoja naye David Luiz

Kwenye dimba la Goodison Park, Everton FC wameibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji Wayne Rooney huku pia kwenye dimba la The Hawthorns, West Bromwich Albiol wakiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bournemouth lililofungwa na Ahmed Hegazy

Crystal Palace wakiwa kwenye dimba lao la Selhurst Park, wamechezea kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa wageni Huddersfield Town mabao ambayo yamefungwa na Steve Mounie pamoja na lile la kujifunga la Joe Ward.

Southampton imelazimishwa sare kwenye dimba la St. Mary’s na Swansea huku Manchester City wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo wa mwisho wa siku ya leo dhidi ya Brighton & Holves Albiol kwa bao la Sergio Aguero na jingine la kujifunga la mchezaji wa Brighton, Lewis Dunk


Spread the love

More in Habari