Connect with us

Habari

Majeruhi Kumuweka Nje Danny Drinkwater Hadi Mwezi Oktoba; Conte Athibitisha

Spread the love

LONDON, Uingereza- Kiungo wa Chelsea, Danny Drinkwater hatoweza kukitumikia kikosi cha Chelsea mpaka mwezi Oktoba kutokana na majeraha ya nyama za nyuma za miguu aliyoyapata siku chache zilizopita.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza alijiunga na Chelsea akitokea Leicester City kwa dau la paundi milioni 35 siku ya mwishi ya usajili

Drinkwater mwenye umri wa miaka 27 alikuwa benchi kwenye mchezo dhidi ya timu yake ya zamani ya Leicester City uliopigwa kwenye dimba la King Power wiki iliyopita huku akishindwa kuwepo kwenye mchezo wa Ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Qarabag

“Maepata maumivu ya misuli kwenyenyama za nyuma za miguu na anahitaji muda ili aweze kupona”, alisema Antonio Conte.

“Nafikiri itakuwa ni ngumu kumuona kabla ya mechi za kimataifa za FIFA. Inasikitisha kwasababu alikuwa ameshaanza kufanya mazoezi na kuimarika kimwili.


Spread the love

More in Habari