Connect with us

Habari

Mahadhi, Ngonyani Safarini Kuelekea Tabora Kukiongezea Nguvu Kikosi Cha Yanga

Spread the love

TABORA, Tanzania- Habari njema kwa wana Yanga ni kuwa wachezaji watano ambao waliachwa jijini Dar es Salaam, wanatarajiwa kuungana na kikosi kizima cha timu hiyo kilichopo mjini Tabora leo.

Yanga iliacha baadhi ya wachezaji wake jijini Dar es Salaam ili kuweza kuwapa muda wa kuimarika kiafya kuelekea mchezo wa Ligi Kuu unaofuata dhidi ya Stand United mwishoni mwa wiki hii sambamba na mchezo dhidi ya Simba Oktoba 28.

Akizungumza na Bin zubeiry Sports, Meneja wa klabu ya Yanga, Hafidh Saleh aliwataja wachezaji hao watakaoungana na wenzao leo kuwa ni pamoja na Ramadhan Kabwili, Pato Ngonyani, Abdallah Hajji ‘Ninja’, Juma Mahadhi na Saidi Mussa.

Licha ya wachezaji hao watano kwenda Tabora leo lakini Saleh ameweka wazi kuwa wachezaji wengine watatu ambao ni Thabani Kamusoko, Donald Ngoma pamoja nae Amissi Tambwe watabaki jijini Dar es Salaam kuendelea na matibabu.

Yanga ipo mjini Tabora kwa ajili ya kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Rhino Rangers inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza ambao utapigwa kesho kwenye dimba la Ali Hassan Mwinyi na baada ya mchezo huo, mabingwa hao wa VPL mara 27 wataendelea na mazoezi wakijiwinda na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Stand United utakaopigwa mjini Shinyanga siku ya Jumapili.


Spread the love

More in Habari