Connect with us

Habari

Lwandamina Aitaka Yanga Kuingia Mawindoni Kusaka Washambuliaji Wa Kati

Spread the love

DAR ES SALAAM, Tanzania- Yanga ipo kwenye mawindo ya kusajili wachezaji wawili wa nafasi ya ushambuliaji ikiwa ni mapendekezo ya kocha George Lwandamina

Yanga siku ya Jumamosi iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliopigwa kwenye dimba la Kaitaba mjini Bukoba lakini hata hivyo bado Lwandamina raia wa Zambia hajaridhishwa na kasi ya upachikaji mabao ya safu yake ya ushambuliaji.

Akiongea na Mwanaspoti, Mwenyekiti wa kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika amekiri kuwa hawakusikiliza ushauri wa kocha wa kutafuta mshambuliaji wa kati kipindi cha usajili lakini sasa hivi wanaona umuhimu wake.

“Unajua ukweli ni kwamba mimi ndiye niliyefanya kazi kwa karibu na Lwandamina wakati wa usajili, kocha aliona uhitaji wa kutafuta straika wa kati, lakini wakati ule hatukutaka kufanya usajili wa kukurupuka, hivyo sasa tumekubaliana naye kwa asilimia zote.

Nafasi ya Msuva

“Ukiangalia kikosi chetu tunatengeneza nafasi, lakini tunafunga chache. Hata ile nguvu yetu ya kufunga tunayoijua haipo na dosari ni kukosa wafungaji hodari, tulimpoteza Msuva ingawa alikuwa winga lakini sote tunajua alikuwa na jicho la ufungaji.

“Kwa sasa hatuna huduma ya Tambwe bado anaugua, huyu ndiye namba tisa pekee tunayemtegemea ongeza na Ngoma naye ameumia, sasa changamoto zote hizo huwezi kumlaumu kocha ni lazima tumtafutie washambuliaji tena wawili wenye ubora, tutavunja benki hakuna namna.

Hata hivyo licha ya kuwa mawindoni kutafuta mshambuliaji wa kati, lakini Nyika alisema pia wanatafuta winga atakayeziba nafasi ya Simon Msuva.

“Pia tutaendelea kutuliza akili kutafuta winga wa kulia mwenye ubora zaidi wa kutengeneza mashambulizi, unajua asili ya mashambulizi ya Yanga ni mawinga, lakini sasa huku namba saba tangu aondoke Msuva bado ingawa tunafurahia kasi ya Buswita anafanya vizuri, lakini ni vyema tukazidi kutafuta.”


Spread the love

More in Habari