Connect with us

Habari

Klabu Bingwa Volleyball Hatua Ya Mtoano Yaanza Kutimua Vumbi Dar, IP Sports Ikiitungua Makongo 3-1

Spread the love

DAR ES SALAAM, Tanzania- Ligi ya mpira wa wavu mkoa wa Dar es Salaam hatua ya mtoano imeanza kutimua vumbi leo kwenye viwanja vya Chuo cha Teknolojia cha DIT Posta jijini Dar es Salaam kwa timu za wanawake na wanaume kuumana.

Mechi hizo za kusisimua zimeanza asubuhi ya leo huku timu nne kwa upande wa wanaume na nne kwa upande wa wanawake zikioneshana umwamba kuelekea katika harakati za kumpata bingwa wa mkoa wa Dar es Salaam kwa mwaka 2017.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye viwanja hivyo vya Chuo cha DIT, timu ya wanawake ya Shule ya Sekondari Makongo iliangukia pua mbele ya Tanzania Prisons ya Ukonga kwa seti 3-1 za 25-21, 17-25, 27-29 na 23-25 huku JKT ikiwafunga kwa mbinde warembo wa timu ya Mji Mwema kutoka Kigamboni kwa seti 3-2 za 25-22, 25-20, 22-25, 12-25, 7-15.

Kwa upande wa wanaume, IP Sports ilianza vyema harakati za kuwania ubingwa huo kwa kuinyuka Makongo Sekondari wanaofundishwa na kocha mzoefu, Yusuf Mkarambati kwa seti 3-1 za 25-17, 17-25, 21-25, na 25-17 katika mchezo wa kulipa kisasi uliokuwa wa kusisimua kwa watazamaji huku katika mchezo wa mwisho wa siku ya leo, Tanzania Prisons wakiitandika JKT kwa seti 3-1 za 24-26, 27-25, 25-21 na 25-20.


Spread the love

More in Habari