Connect with us

Habari

Kivumbi Cha Mzunguko Wa Tatu Ligi Kuu Ya Vodacom Kuanza Leo; Tazama Hapa Kujua Nani Atacheza Na Nani

Spread the love

DAR ES SALAAM, Tanzania- Mzunguko wa tatu wa Ligi Kuu ya Vodacom unatarajiwa kuendelea mwishoni mwa wiki hii ambapo timu mbalimbali zitashuka dimbani kuoneshana umwamba katika kuwania alama tatu muhimu ili kuendelea kujiimarisha kwenye msimamo wa Ligi

Mzunguko wa tatu utafunguliwa kwa mechi kali nay a kusisimua itakayopigwa leo Ijumaa Septemba 15, ambapo Azam FC itaialika Kagera Sugar muda mfupi kuanzia sasa katika dimba la Azam Complex katika mchezo unaotarajiwa kuwa wa vuta nikuvute kutokana na rekodi ya timu hizo zote mbili.

Kwa siku ya Jumamosi Septemba 16, 2017 Majimaji FC ya Songea itacheza na Young Africans ya Dar es Salaam, saa 10.00 jioni katika Uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma.

Mbao itasafiri hadi Manungu mkoani Morogoro kucheza na Mtibwa Sugar katika mchezo ambao pia utapigwa Jumamosi saa 10 jioni wakati Tanzania Prisons ya Mbeya itakuwa mwenyeji wa Ndanda FC saa 16h00 kwenye Uwanja wa Sokoine.

Lipuli Fc itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting saa 10 jioni katika Uwanja wa Samora, Iringa wakati Stand United itacheza na Singida United saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Siku ya Jumapili Septemba 17, 2017 Mbeya City itaikaribisha Njombe Mji saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya huku Simba SC ikiwa mwenyeji wa Mwadui FC saa 10 jioni katika Uwanja wa Uhuru, Dar es salaam.

Mpaka sasa Mtibwa Sugar ndio anaongoza msimamo wa ligi akiwa na alama sita baada ya kuibuka na ushindi kwenye michezo miwili mfululizo huku Simba wakishika nafasi ya pili wakiwa na alama nne wakizipita timu nyingine zenye alama nne kwa wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.


Spread the love

More in Habari