Connect with us

Habari

Harry Kane Atakuwa Fiti Kuivaa Arsenal; Pochettino Athibitisha

KOCHA wa Spurs, Mauricio Pochettino amethibitisha kuwa Harry Kane atakuwa tayari kuivaa Arsenal kwenye London derby itakayopigwa Novemba 18 mwaka huu kwenye dimba la Emirates.

Kane ameachwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kinachotarajiwa kucheza dhidi ya Ujerumani na Brazil kwenye michezo ya kimataifa ya kirafiki wiki hii kufuatia mazungumzo kati ya wataalam wa tiba wa klabu yake na kocha wa timu ya taifa Gareth Southgate.

Mshambuliaji huyo amekuwa akiuguza maumivu ya misuli ya paja ambayo yalimfanya kuukosa mchezo dhidi ya Manchester United Oktoba 28 ambao timu yake ililala kwa bao 1-0 pamoja na ule dhidi ya Crystal Palace siku ya Jumapili ambao waliibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0.

“Harry Kane yupo vizuri. Alipata dhoruba kwenye goti lake lakini msijali atakuwepo kwenye mechi inayofuata,” alisema Pochettino kwenye sherehe za uzinduzi wa kitabu kipya cha mwandishi Guillem Balague.

Spurs wana alama nne juu ya Arsenal kwenye msimamo wa EPL huku wanashikilia nafasi ya tatu nyuma ya Manchester United na Manchester City.

More in Habari