Connect with us

Habari

Arsenal Na Cologne Zafunguliwa Mashtaka Na UEFA Kutokana Na Vurugu Za Mashabiki

Spread the love

NYON, Uswisi- Cologne na Arsenal zimefunguliwa mashtaka na Shirikisho la soka barani Ulaya, UEFA kutokana na vitendo vya vurugu vilivyofanywa na mashabiki wao kwenye mchezo wa jana wa Europa League

Klabu ya Cologne kutoka nchini Ujerumani inakabiliwa na mashtaka manne ikiwemo vurugu za mashabiki wao, kuwasha moto, kurusha vitu vyenye kuhatarisha usalama pamoja na uharibifu huku Arsenal wakikabiliwa na shtaka la kufunga njia za ngazi kwenye uwanja.

Mechi hiyo ilicheleweshwa kwa zaidi ya saa moja kutokana na maelfu ya mashabiki wa Cologne kufika kwenye uwanja wa Emirates bila kuwa na tiketi.

Takribani mashabiki 20,000 wa Cologne walifika jijini London kuhudhuria mchezo huo licha ya kupewa tiketi 2900 tu huku kesi hiyo ikitarajiwa kusimamiwa na bodi ya usimamizi wa nidhamu na maadili ya UEFA siku ya Septemba 21

Arsenal kwa upande wao wametoa taarifa siku ya leo ambayo inasomeka; “Tulitaarifiana na wenzetu wa Cologne kuwazuia mashabiki waliokuwa wakisafiri bila tiketi.

“Tiketi 3000 zilitolewa kwa mashabiki wa Cologne kutokana na sheria za mashindano lakini ni wazi kuwa mashabiki wengi waliwasili ambapo walisababisha usumbufu mkubwa nje ya uwanja kabla ya mchezo kuanza. Tiketi nyingi ziliuzwa kiholela na jambo hili limetusikitisha.

Arsenal ilitoka nyuma na kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 kwenye mchezo huo wa Europa League kundi H huku mabao ya Arsenal yakifungwa na Saed Kolasinac, Alexis Sanchez na Hector Bellerin huku bao la kufutia la machozi la wageni likifungwa na Jhon Cordoba

 


Spread the love

More in Habari