Connect with us

Habari

Arsene Wenger: Ozil Na Sanchez Wanaweza Kuondoka Januari

ARSENE WENGER ameweka wazi kuwa mazungumzo kati ya Arsenal, Mesut Ozil na Alexis  Sanchez kuhusu kusaini mikataba mipya yanaendelea vizuri ingawa wachezaji hao wanaweza kuondoka mwezi Januari.

Mikataba ya Mesut Ozil na Alexis Sanchez inategemewa kumalizika mwishoni mwa msimu uliopita.

Alipotakiwa kuthibitisha taarifa kuwa mazungumzo na wakala wa Ozil yanaendelea vizuri, Wenger alisema; “Hilo ndio suala ninalolijua.

“Kutokana na kutokukubaliana msimu uliopita haimaanishi kuwa anataka kuondoka.”

“Wachezaji wote wanaonekana kuwa na furaha, hali inaweza kubadilika lakini kwa sasa hatupo karibu kuthibitisha chochote. Mazungumzo yanaendelea vizuri.

Hata hivyo Wenger alipoulizwa uwezekano wa Ozil na Sanchez kuuzwa dirisha la usajili likifunguliwa, alisema: “Ukiwa unakumbwa na hali kama tunayokutana nayo sasa ungekubaliana na hali yoyote, ndio. Inawezekana.”

More in Habari