Connect with us

Habari

Amerudi: Danny Usengimana Arejea Mazoezini Singida United Baada Ya Kupona Majeraha Ya Mguu

Spread the love

SINGIDA, Tanzania- Mshambuliaji wa klabu ya Singida United, Danny Usengimana amerejea uwanjani baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yanamsumbua.

Usengimana aliyesajiliwa na Singida United akitokea klabu ya Polisi ya nchini Rwanda alikuwa nje ya uwanja akisumbuliwa na matatizo ya kifundo cha mguu ambapo alikosa mechi mbili za kwanza za Ligi Kuu ya Vodacom ambazo SIngida United walicheza dhidi ya Mwadui FC na Stand United.

Akizungumza na tovuti ya Saleh Jembe, Usengimana ambaye ametwaa kiatu cha ufungaji bora kwenye Ligi Kuu ya Rwanda kwa misimu miwili mfululizo amesema yupo fiti na ana matarajio ya kuanza kwenye mchezo unaofuata wa Ligi Kuu.

“Namshukuru Mungu nimepona majeraha ya mguu yaliyokuwa yakinisumbua, na tayari nimeanza mazoezi kwa ajili ya kuitumikia timu yangu na natarajia kucheza mechi ijayo ya ligi.

Kufunga

Akizungumzia matarajio yake kwenye msimu huu mpya wa Ligi, Usengimana amedai kuna ana kibarua kikubwa cha kufanya kuhakikisha anaisaidia Singida United kufanya vizuri.

“Kazi yangu ni kufunga na nataka niendelee kufunga kama ilivyokuwa kule nilipotoka kwa ajili ya kuisaidia timu yangu kufikia malengo,” alisema Usengimana.

Hata hivyo mshambuliaji huyo atakuwa na kazi kubwa katika mbio za kuwania kiatu cha ufungaji bora dhidi ya washambuliaji wa vilabu mbalimbali vya Ligi Kuu hususani Emmanuel Okwi ambaye tayari ameshafunga mabao manne kwenye mechi moja aliyocheza.

Usengimana amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Singida United inayodhaminiwa na SportPesa na tayari ameshaonesha kiwango kizuri katika mechi za majaribio ikiwemo mechi dhidi ya Yanga iliyopigwa kwenye dimba la Taifa Agosti 11 ambapo alifunga bao moja licha ya timu yake kupokea kichapo cha mabao 3-2


Spread the love

More in Habari