Connect with us

Habari

Aguero Atamani Kumuona Messi Ndani Ya Uzi Wa Man City

MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Sergio Aguero amekiri kwamba angependa kumuona Lionel Messi anasajiliwa klabuni hapo lakini hata hivyo amesema kuwa usajili huo utakuwa na utata mwingi

Dau la kumng’oa Messi Barcelona ni paundi milioni 268.7 kulingana na mkataba wake unavyodai lakini Aguero anaamini kama Messi atakuwa na nia ya dhati ya kujiunga na Man City, pesa itakuwa sio tatizo.

“Nafikiri Messi kama alivyo Cristiano Ronaldo ni wachezaji ambao ni nembo kwenye vilabu vyao na ni vigumu kwa wao kuhamia vilabu vingine.

“Ningependa kumuona Messi kwenye timu yangu, lakini ni vigumu sana,” alisema Aguero ambaye usiku wa kuamkia jana alimshuhudia Messi akifunga mabao matatu dhidi ya Equador na kuiwezesha Argentina kufuzu kwa kombe la dunia mwakani nchini Urusi.

More in Habari